KOCHA MAURIZIO SARRI KATAJA SABABU ZA JUVENTUS KUTAKA KUMUUZA DYBALA
Kipindi hiki cha usajili kimekuwa kikimuhusisha sana mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala kuuzwa na Juventus ambapo vilabu vya Ligi Kuu ya England kama Manchester United na Tottenham Hotspurs vilimfukizia lakini wakashindwa kumnasa mpaka dirisha linafungwa nchini England.
Kutaka kuuzwa kwa Paulo Dybala ndani ya Juventus kulikuwa kunawapa maswali baadhi ya watu huku wengine wakihoji kwa nini kocha Maurizio Sarri anafikiria kufanya uamuzi kama huo.
Maurizio Sarri ameweka wazi sababu ya Juventus kufanya hivyo ni kutokana na kutaka kupunguza wachezaji 6 ili kuendana na matakwa ya UEFA katika michuano ya Ligi ya Mabingwa japokuwa anaona Dybala bado anaweza kuwa na mchango katika kikosi chake.
.
“Kuna wakati unachoka kabisa unapokuwa unasoma magazeti (Kutaka kuuzwa kwa Dybala) eti ni kutokana na machaguo ya Sarri, umekiangalia kikosi cha Juventus? tunatakiwa kupunguza wachezaji sita ili kufikia orodha ya idadi ya wachezaji wanaohitajika katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, habari ambayo sijaiona ikiandikwa popote”
.
“Tunatakiwa kupunguza wachezaji sita katika kikosi cha sasa maamuzi ambayo yananiweka katika wakati mgumu, siku 20 za mwisho za dirisha la usajili zitakuwa ngumu kwetu kwa sababu tunatakiwa kufanya maamuzi ya hatari ya kuacha wachezaji waondoke ambao ni wa kiwango cha juu kwetu”