ANTONY JOSHUA NA RUIZ JR KURUDIANA SAUDI ARABIA
Kukiwa na mvutano juu ya wapi pambano la marudio baina ya bondia Antony Joshua na Andy Ruiz Jr sasa nchi ya Saudi Arabia imetajwa kuwa sehemu watakapopambania mabondia hawa.
Joshua alipoteza mikanda ya IBF, WBA na WBO kwa Ruiz na wawili hawa wamekuwa wakivutana juu ya mahala pambano la marudio litakapopigwa.
Saudi Arabia inaonekana ikiweza patiwa dhamana kuandaa pambano hilo la marudiano kwani nchi hiyo tayari imekwisha andaa mapambano kadhaa ya ubingwa wa dunia huku hivi karibuni bondia Amir Khan akiwa amepigana pambano lake dhidi ya Billy Dub nchini humo