Mwanadada wa Ufaransa kuweka Historia UEFA
UEFA imemtangaza mwanadada Stephanie Frappart kuwa mwamuzi wa mchezo wa UEFA Super Cup kati ya Liverpool na Chelsea utakaopigwa Agosti 14,2019 Vodafone Arena mjini Istanbul,Uturuki.
Stephanie anaweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuchezesha mechi ya wanaume ya UEFA.
Mfaransa huyo,35, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa mechi ya fainali ya kombe la Dunia la wanawake mwaka huu iliyozikutanisha USA na Uholanzi.