Familia ya Solskjaer yaandika Historia nchini kwao Norway
Usiku wa jana klabu ya Manchester United ikiwa chini ya kocha wao Ole Gunnar Solskjaer ilikuwa Norway kucheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya Kristiansund.
Mchezo huo ulimalizika kwa Kristiansund kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Manchester United lakini kivutio kikubwa kilikuwa ni kwa Noah Solskjaer ambaye ni mtoto wa kocha wa sasa wa Manchester United.
Noah ,19, alipata nafasi ya kucheza mechi hiyo akiingia dakika ya 85 ikiwa ni mechi yake ya kwanza ya timu ya wakubwa.
Wakati Noah akiingia uwanjani baba yake,Ole Gunnar Solskjaer aliinuka kwenda kumpongeza mwanae.
Noah alifahamika zaidi 2004 kupitia baba yake Ole Gunnar Solskjaer kwa kupenda kuingia nae uwanjani enzi hizo akiichezea Man United.

Wakati wa mchezo huo wa jana Ole Gunnar Solskjaer pia alikuwa kaongozana na mwanae mwingine mdogo Elia.