Rodgers hana presha na Man United
Klabu ya Manchester United moja kati ya nafasi inazodaiwa kukusudia kuziimarisha kabla ya kuanza kwa msimu huu ni pamoja na nafasi ya beki wa kati licha ya kukutana na vizuizi.
Kwa sasa Manchester United inahusishwa kwa karibu kutaka huduma ya beki wa Leicester City Harry Maguire ila wanashindwa kufikia dau la karibia Pauni milioni 80 zinazohitajiwa na Leicester City.
Kocha wa Leicester City Brendan Rodgers ambaye awali ilikuwa inaripotiwa kuwa anahimiza uongozi kuwa kama wanampango wa kumuuza Maguire wafanye maamuzi hayo mapema ili atafute mbadala wake, ameonekana hana presha tena na hilo kutokana na kauli anazozitoa.
.
“Kiukweli sifikirii kabisa kuhusiana na hilo tumebakiza wiki mbili kuelekea kufungwa kwa dirisha la usajili la wachezaji wote, ninafikiri ni suala la kila mmoja kuangalia alipokusudia” alisema Rodgers
.
“(Maguire) amekuwa na akionesha kiwango toka siku ya kwanza ya maandalizi ya msimu na amekuwa akihusishwa na tetesi nyingi lakini wote tume-relax na tunaiandaa timu na Maguire ni sehemu ya timu” aliongezea Rodgers
Kauli ya Rodgers imetafsiriwa na baadhi ya wachambuzi kuwa anaamini kwa siku zilizosalia uhamisho wa Maguire kwenda Man United hauwezi kutokea, kauli hiyo aliitoa katika mchezo wa kirafiki uliomalizika kwa Leicester kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Stoke City.