Masoud Juma asajiliwa Algeria
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Kenya Harambee stars Masoud Juma amekamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya JS Kabylie inayoshiriki ligi kuu nchini Algeria.
Mshambuliaji huyo,23,amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu ikiwa imepita miezi kadhaa tangu avunje mkataba na timu ya Al-Nasr Benghazi ya nchini Libya.
.
“ Tunafuraha kutangaza kumsajili mshambuliaji wa Kenya kwa mkataba wa miaka mitatu” Klabu hiyo ya Algeria imeandika katika tovuti yao.
Juma aliwahi kushinda tuzo ya mfungaji bora mwaka 2017 katika ligi kuu nchini Kenya akiwa na timu ya Kariobang Sharks.