Ukata wa pesa wawanyima Fernabahce kumsajili Mesut Ozil
Baada ya kuibuka tetesi kuhusu klabu ya Fernabahce kutaka kumsajili kiungo wa Arsenal Mesut Ozil,klabu hiyo imetoa taarifa rasmi kuwa wapo katika hali mbaya ya kiuchumi hivyo hawana uwezo wa kumnunua mchezaji huyo.
Mesut Ozil,30, ndiye mchezaji anayelipwa zaidi Arsenal, akipokea Pauni 350,000 (Tsh Bilioni 1) kwa wiki baada ya kusaini mkataba mpya mwaka jana.