TFF kusomesha wachezaji wa timu za vijana
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania ‘TFF’ limeingia udhamini wa kudumu na shule ya Fountain Gate iliyopo jijini Dodoma kwa kuwasomesha Vijana waliopo katika timu za taifa za umri chini ya miaka 13,15 na miaka 17.
Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo Athumani Nyamlani amesema kuwa katika shule hiyo Vijana watapata Elimu ya kimaadili ya darasani na Elimu ya kimaadili ya mpira.
Mkurugenzi Mkuu wa shule hiyo Japhet Makau amesema kuwa wameamua kuiunga mkono TFF na wamejiandaa kuhakikisha vijana hao wanapata Elimu iliyo bora katika shule hiyo.