Msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara kuanza Agosti 23
Bodi ya Ligi kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo,Boniface Wambura ametangaza tarehe ya kuanza kwa Ligi kuu Tanzania bara ambapo itaanza August 23 mwaka huu na kumalizika Mei 24 mwaka 2020.
Wambura amesema kuwa ratiba ya Ligi kuu Tanzania bara imetolewa kwa kuzingatia upangaji wa timu zinapo kutana ilikupunguza ghalama kwa timu pindi zinapoenda kucheza katika viwanja tofauti tofauti.