Amunike afutwa kazi Taifa Stars
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefikia makubaliano na aliyekuwa kuwa Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania“Taifa Stars” Emmanuel Amunike ya kusitisha mkataba baina yao.
Amunike alijiunga kuwa Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘ Taifa Stars’ August 6 mwaka 2018 ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili.
Kocha huyo aliiwezesha Taifa Stars kufuzu fainali za AFCON zinazoendelea nchini Misri hii ambapo Tanzania ndio timu ya kwanza ilotolewa katika michuano hiyo,na hii ni baada ya miaka 39 kupita tangu Tanzania ifuzu fainali hizo.