Simba yaingia mkataba na kinywaji cha Mo Xtra
Klabu ya Simba imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na kampuni ya A one kupitia kinywaji cha MO xtra baada ya mkataba wa awali kumalizika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu hiyo Crescentius Magori amesema kuwa mkataba huo una thamani ya shilingi milioni 250, na kampuni ya A one ni mdhamini mkubwa sana ndani ya Klabu ya hiyo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya MeTL Group Fatema Dewji amesema kuwa walipata mafanikio makubwa kwa kuidhamini Simba SC kwa mwaka mmoja, na kwa mwaka huu wameamua kuendeleza ushirikiano huo na mabingwa hao wa Tanzania.