Rostam amwaga mamilioni Yanga
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ambaye ameahidi kuichangia Yanga Tsh Milioni 10, amesema kuwa Mfanyabiashara Rostam Aziz ambaye yupo nchini Marekani, ameahidi kuichangia timu hiyo Tsh Milioni 200. Majaliwa ameyasema hayo leo wakati wa sherehe ya uchangishaji ya Yanga iliyofanyika Diamond Jubilee Dar es salaam.