Msolla awapa onyo wanautumia nembo ya Yanga vibaya
Klabu ya Yanga kupitia kwa mwenyekiti wa Klabu hiyo Mshindo Msolla imewatak wale wote wanaotumia nembo ya Yanga kutengeneza jezi wafike makao makuu ya Klabu hiyo ili waweze kufanya mazungumzo. Msolla pia amewataka wale wanaotumia mitandao ya kijamii kwa jina la Klabu ya Yanga waache tabia hiyo maana klabu hainufaiki chochote kupitia mitandao hiyo .