Jackson Mayanja atua KMC
Baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa Klabu ya KMC Etienne Ndayiragije kuondoka na kujiunga na Klabu ya Azam, KMC imemnasa aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Klabu ya Simba SC Jackson Mayanja kwa mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Klabu hiyo.
Uongozi wa KMC kupitia kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amesema kuwa wanaimani na Kocha Mayanja kutokana na CV yake na wanaamini ataifikisha KMC mahali wanapo tarajia kufika hasa katika michuano ya kimataifa.