Maajabu yatokea mechi ya Mali na Mauritania AFCON
Katika mechi ya jana ya AFCON 2019 ya kundi E ambayo Mali waliibuka na ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Mauritania, timu ya Taifa ya Mali ilikuwa na wachezaji wawili ambao wote wanaitwa Adama Traore.
Adama Traore mmoja alianza na mwingine akawa benchi.
Dakika ya 55 ya mchezo yule Adama Traore aliyeanza alifunga goli, ilivyofika dk 61 akatolewa na nafasi yake kuchukuliwa na yule Adama Traore aliyekuwa benchi, na yeye alivyoingia akafanikiwa kufunga goli dk 74 ya mchezo.

Wachezaji hawa si ndugu, wote wanacheza Ligue 1, mmoja anacheza Metz na mwingine AS Monaco.