Ofisi za TFF sasa zapelekwa Kigamboni
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF linatarajia kuhamisha ofisi zake zilizopo Ilala Karume jijini Dar es Salaam na kwenda Kigamboni ifikapo Disemba mwaka huu.
Hayo yamesemwa na makamu wa Rais wa Shirikisho hilo Athumani Nyamlani wakati wa zoezi la kukabidhiwa Uwanja na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Uwanja huo upo Kigamboni Jijini Dar es Salaam wenye ukubwa wa Hekari 15 na una thamani ya bilioni 1.5
Uwanja huo ni kwa ajili ya kujenga shule/kituo cha soka kwa lengo ili kuendeleza kukuza vipaji na kupata wachezaji wazuri wa timu za taifa.
Nyamlani amemshukuru Makonda na kumuahidi kuwa ujenzi huo utaanza muda mfupi ujao kwa sababu pesa za ujenzi wanazo, walipewa na FIFA kwa ajili ya kuendeleza michezo nchini. ” Kwa niaba ya TFF ninapenda kumshukuru sana Mh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kutupatia uwanja huu ambao tulikuwa tunauhitaji kwa muda mrefu lakini tulishindwa kutokana na gharama kuwa kubwa,hii ni moja ya chachu ya maendeleo ya michezo hapa nchini kwetu,Mungu akipenda hadi Disemba mambo yakikamilika TFF yote tutahamia Kigamboni” Nyamlani