Platini atolewa mahabusu
Aliyekuwa Rais wa UEFA Michel Platini ambaye alikamatwa jana, ameachiliwa na Polisi wa Ufaransa leo Jumatano mapema asubuhi baada ya kuhojiwa kwa muda wa saa 15.
Platini,63, alikamatwa jana na kuwekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kupokea rushwa na kuipa Qatar nafasi ya uenyeji wa kombe la Dunia Mwaka 2022.
Baada ya kutolewa Platini ameeleza kuwa hakuna shitaka lolote ambalo amepewa.
.
“ Mara zote nimekuwa mtulivu kwa sababu ninajihisi ni mgeni katika matatizo haya.
.
Nilipaswa kuingia nikiwa huru, niliwasili na mara tu nikipelekwa mahabusu. Inaumiza kwa kila kitu ambacho nimefanya, inaumiza.”
.
Lakini, wamefanya kazi yao na tumejaribu kujibu maswali yote.” Amesema Platini baada ya kuachiwa huru.