Rais wa UEFA apelekwa mahabusu
Rais wa zamani wa UEFA Mfaransa Michel Platini amekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi kwa kesi ya kuhusiana na kuipa Qatar nafasi ya uenyeji wa kombe la Dunia mwaka 2022.
Platini,63, alichaguliwa kwenye kiti hicho cha Urais mwaka 2007 na kutumikia mpaka mwaka 2015 ambapo alifungiwa na kamati ya nidhamu ya FIFA kwa mlolongo wa makosa.
Imeelezwa kuwa Platini leo asubuhi amechukuliwa na kupelekwa kizuizini ikiwa ni sehemu ya uchunguzi kuhusu kutoa wenyeji wa kombe la Dunia kwa Qatar mwaka 2022.
Disemba 2010 Qatar walitangazwa kushinda uenyeji wa michuano ya kombe la Dunia mwaka 2022, lakini kumekuwa na utata juu ya ushindi huo huku ikielezwa rushwa ilifanyika ili nchi hiyo kupata nafasi hiyo ya uenyeji.