Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewapa klabu ya Yanga uwanja huko Kigamboni, ambapo klabu hiyo kupitia mwenyekiti wake Mshindo Msolla wamesema watautumia uwanja huo kujenga kituo (Academy) ya kukuza vipaji. Makonda ametoa ahadi hiyo katika hafla ya uchangishaji ya timu hiyo iliyofanyika leo Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Day: June 15, 2019
Rostam amwaga mamilioni Yanga
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ambaye ameahidi kuichangia Yanga Tsh Milioni 10, amesema kuwa Mfanyabiashara Rostam Aziz ambaye yupo nchini Marekani, ameahidi kuichangia timu hiyo Tsh Milioni 200. Majaliwa ameyasema hayo leo wakati wa sherehe ya uchangishaji ya Yanga iliyofanyika Diamond Jubilee Dar es salaam.