Sasa Tanzania kupeleka timu 4 mashindano ya kimataifa
Tanzania itapeleka timu nne katika michuano ya kimataifa msimu ujao 2019/20,shirikisho la soka barani Afrika CAF limethibitisha.
Tanzania imepewa nafasi hizo nne kufuatia kuwa katika nafasi 12 bora kwenye viwango vya ubora vya CAF.
Shirikisho la soka nchini Tanzania limeeleza kuwa kwa mujibu wa za ligi kuu zilizofanyiwa marekebisho na kamati ya utendaji, timu zitakazoshiriki michuano hiyo ni Simba SC na Yanga SC ambazo zitacheza ligi ya mabingwa , na Azam pamoja na KMC waliomaliza nafasi ya nne watashiriki kombe la shirikisho.