Senegal waweka Bilioni 11 kwa ajili ya AFCON
Timu ya taifa ya Senegal inaelekea wamejipanga kumaliza ukame wa kihistoria wa kutowahi kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON, Senegal ambayo imepangwa Kundi C pamoja na Tanzania, Algeria na Kenya wanashauku ya kutaka kutwaa taji hilo na wameanza maandalizi makubwa.
Kuelekea kuanza kwa fainali hizo ambapo zimebaki siku ya 22 waziri wa michezo wa Senegal, Mr Matar Ba katangaza bajeti ya dola milioni 5.1 ambayo ni sawa na zaidi ya Tsh Bilioni 11 za kitanzania kwa ajili ya kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri katika michuano hiyo.
Senegal imetenga kiasi hicho kwa ajili ya kutumika katika maandalizi ya michuano pamoja na posho za wachezaji.
Timu hiyo itakaweka kambi yao watakayoweka nchini Hispania kujiandaa na fainali hizo zitazochezwa nchini Misri mwaka huu kuanzia Juni 21 mpaka Julai 19.