Giroud awapa heshima Maboss wake wa zamani
Usiku wa fainali ya Europa League ilikuwa ni usiku wa kihistoria kutokana na kukutanisha timu za Arsenal naChelsea ambazo sio tu zinatoka taifa moja bali jiji moja la London hawa ni majirani kweli kweli.
Kingine cha kuvutia ni kuwa Arsenal ilikuwa na mlinda mlango wa zamani wa Chelsea Petr Czech lakini safu ya ushambuliaji ya Chelsea ilikuwa inaongozwa na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Oliver Giroud aliyeanza kwa kukata utepe wa magolikwa kuifungia Chelsea bao la kwanza katika ushindi wa4-1.
Giroud aliyecheza Arsenal kwa miaka sita (2012-2018) baada ya kufunga goli hilo alishindwa kushangilia nakupiga magoti huku akionesha ishara ya kuomba radhi kwa kuifunga timu yake ya zamani, kilichomfanya asishangilie na ajisikie vibaya ni kutokana anaamini ameondoka Arsenal akiwa ana deni la kuipa mafanikio.
“Nadaiwa na Arsenal sana ndio maana sikutaka hata kushangilia nilivyofunga goli japo kwa upande mwingine najivunia kushinda taji hili nikiwa na Chelsea, ni wazi mimi ni Chelsea (The Blues) wa ukweli” kauli ya Oliver Giroud baada ya mchezo huo.