Eden Hazard awaaga Chelsea
Baada ya ushindi wa mabao 4-1 wa Chelsea dhidi ya Arsenal katika mchezo wa fainali ya Europa League iliyochezwa katika uwanja wa Olympic mjini Baku katika nchi ya Azerbaijan, Eden Hazard ameweka wazi msimamo wako na kutoa kauli inayoashiria safari yake Stamford Bridge imefikia mwisho.
Hazard ambaye katika mchezo huo alisaidia kwa kiwango kikubwa kupatikana kwa ushindi huo kwa kufunga magoli mawili na kutoa pasi moja ya usaidizi wa goli, baada ya mchezo huo aliulizwa kuwa vipi hiyo ndio kwa heri kwa Chelsea au kuna kingine? Hazard anahusishwa kwa kwango kikubwa kujiunga na Real Madrid kipindi hichi mkataba wake unapomalizika.
.
“Tayari nimeshafanya maamuzi na navisubiri vilabu vyote tu, nafikiri hii ni ndio kwa heri lakini katika mchezo wa mpira hauwezi kujua labda kwa sasa ndio muda muafaka wa kutafuta changamoto mpya” alisema Hazard ambaye amecheza michezo 352 akiwa Chelsea na kufunga mabao 110 na pasi 92 za usaidizi akishinda mataji mawili ya EPL, mawili ya Europa League na moja la FA Cup.