Unai Emery afichua ugumu wa maisha yake ya Paris
Moja ya mitihani mikubwa wanayokumbana nayo makocha na wachezaji wanapoamua kutoka katika maisha yao ya soka katika nchi zao na kwenda kutafuta maisha katika mataifa mengine ni suala la lugha, wachache sana ambao wamekuwa na umahiri wa kuzungumza lugha zaidi ya moja.
Kocha wa sasa wa Arsenal Unai Emery ameweka wazi kuwa amewahi kukumbana na wakati mgumu akiwa nchini Ufaransa kwa misimu miwili, Unai ni Mhispania aliyezaliwa Hondarribia na lugha yake ya kwanza ni kihispanyola, hivyo alivyokuwa PSG katika jiji la Paris nchini Ufaransa alikuwa akipata tabu kuzungumza kifaransa na badala yake alikuwa akiambulia kuchekwa kwa kuongea kwa kukosea kosea.
Mambo yamekuwa tofauti England na badala yake amekuwa akipokelewa vizuri anapokuwa anazungumza broken English na hachekwi tena kama ilivyokuwa Ufaransa, hivyo amekuwa akifurahia zaidi maisha yake ya London England akiwa anaifundisha Arsenal, Unai anakumbana na changamoto hiyo kutokana na katika maisha yake ya uchezaji soka hajawahi kucheza nje ya Hispania.
.
“Heshima ndio kitu cha kwanza unajisikia raha kuwa hapa (Arsenal) ,nilipowasili Paris (PSG) nilikuwa najaribu kuzungumza kifaransa lakini watu wakawa wananibeza (wananicheka) kwa sababu sijui vizuri ila London nazungumza broken English lakini kila mmoja anafuraha na jitihada zangu”
Arsenal ndio timu yake ya tatu kuifundisha ya nje ya Hispania baada ya Spartak Moscow aliyokaa miezi kadhaa (2012) na PSG (2016-2018), kocha wa Arsenal aliyepita Arsene Wenger alikuwa na uwezo wa kuzungumza lugha sita (Kifaransa, Kijerumani, Kiingereza, Kihispanyola na Kijapan na kiitaliano)