Mtanzania asajiliwa Blackpool Uingereza
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Adi Yussuf amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu ya Blackpool katika majira haya ya kiangazi akisajiliwa kwa muda wa miaka miwili huku kukiwa na chaguzi ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja. Mchezaji huyo,27, anajiunga na timu hiyo inayoshiriki League One nchini England akitokea Solihull Moors ambayo inayoshiriki National League …