Hamilton ashinda Monaco Grand Prix
Ni Lewis Hamilton wa Mercedes ndiye ameibuka mshindi wa Monaco Grand Prix leo, Sebastian Vettel wa Ferrari akishika namba mbili huku Valtteri Bottas akimaliza nafasi ya tatu.
Max Verstappen wa Red Bull alimaliza nafasi ya pili lakini baadae akashushwa mpaka nafasi ya nne kufuatia kupata penati ( 5 second time penalty)
.
Ushindi huu unamfanya Hamilton aendelee kuongeza pointi katika kuongoza msimamo wa madereva msimu huu ambapo amefikisha pointi 137 huku dereva mwenzake wa Mercedes Valtteri Bottas akiwa nafasi ya pili na pointi 120.