Mvua zazuia sherehe za Simba Dar
Kutokana na mvua kubwa kunyesha leo jijini Dar es Salaam katika mchezo wa leo ambao ulikuwa maalumu kwa Klabu ya Simba SC kukabidhiwa Kombe la Ubingwa leo zoezi hilo limeahirishwa mpaka wiki ijayo Mei 28.
Simba SC sasa atakabidhiwa Kombe hilo kwenye mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Jumanne ijayo Mei 28 kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Msemaji kwa Klabu hiyo Haji Manara amesema kuahirishwa kwa sherehe hizo kumetokana na mvua hizo zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
.
” Sherehe za kukabidhiwa kombe sasa zitafanyika Morogoro siku ya Jumanne tarehe 28 tutakapocheza na Mtibwa Sugar,
kuhairishwa huku kumetokana na mvua kubwa kuendelea kunyesha hapa Dar es Salaam ambayo itawakosesha Wanasimba kukosa uhondo wa kukabidhiwa kombe lao la ubingwa wa ligi kuu” Manara