Lugola kuwakabidhi Ubingwa Simba
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kesho Mei 25 ,kwenye mechi ya Ligi kuu Tanzania bara kati ya Simba SC na Biashara United.
Mchezo huo utachezwa saa 9.00 Alasiri kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Clifford Ndimbo amesema mchezo huo utatumika kuwakabidhi Kombe la Ubingwa Simba SC ambao ndio mabingwa wa msimu huu wa 2018/19.
Ikumbukwe kuwa Simba SC hii ni mara ya 20 kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu, huku watani wake wa jadi Yanga SC wakiwa wamechukua Ubingwa wa Ligi Kuu mara 27.