Ligi Tanzania Bara kuchezwa kesho saa mbili asubuhi
Baada ya kuahirishwa kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara kati ya JKT Tanzania na Kagera Sugar sasa mchezo huo kuchezwa kesho.
Mchezo huo ulitakiwa uchezwe jana Mei 23 lakini uliahirishwa kutokana na Uwanja wa Isamuhiyo wanaoutumia JKT Tanzania kama Uwanja wao wa nyumbani kuwa mbovu.
Mchezo huo utachezwa kesho saa 2.00 asubuhi kwenye Uwanja wa JK Park uliopo maeneo ya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam ,amethibitisha Kocha mkuu wa Kagera Sugar Mecky Maxime kupitia EFM radio.