Siasa zamkosesha fainali Mkhitaryan
Kwa sababu za kiusalama klabu ya Arsenal imethibitisha kiungo wao Henrikh Mkhitaryan hatasafiri na timu hiyo kuelekea mjini Baku,Azerbaijan katika fainali ya Europa League dhidi ya Chelsea itakayochezwa Mei 29,2019.
.
Kiungo huyo wa Armenia anakosa mchezo huo kutokana na uhasama wa kisiasa uliopo kati ya Taifa lake na nchi ya Azerbaijan.
Oktoba mwaka jana kiungo huyo alikosa mechi dhidi Qarabag iliyochezwa Baku kwa sababu hiyo hiyo kwa kiusalama.
Armenia na Azerbaijan kwa muda mrefu wamekuwa wakigombania eneo Nagorno-Karabakh ambalo kwa wingi limetawaliwa na milima na misitu.
.
“Tumefanya kila njia kwa ajili ya Mkhitaryan kuwa sehemu ya kikosi lakini baada ya kujadiliana na Micki na familia yake kwa pamoja tumekubaliana hatakuwa sehemu ya watakaosafiri” wametoa taarifa hiyo Arsenal.
.
Kupitia akaunti yake ya Instagram Micky ameeandika kwa majonzi makubwa kueleza kusikitishwa kukosa fainali hiyo.
“ Ni aina ya mchezo ambao hauji mara kwa mara kwa sisi wachezaji na lazima nikiri inaniumiza sana kuukosa.”