Azerbaijan wamjibu Jurgen Klopp
Chama cha soka cha Azerbaijan kimemjibu kocha wa Liverpool Jurgen Klopp aliyekosoa UEFA kwa kuipeleka fainali ya Europa Ligi msimu huu mjini Baku nchini Azerbaijan.
.
Kocha huyo ambaye timu yake inacheza fainali ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Tottenham jijini Madrid, alisema kuwa hajui ni kifungua kinywa gani walipata watu wa UEFA kabla ya kufanya maamuzi hayo ya kuipeleka fainali ya Europa Ligi Baku, akieleza kuwa ni mbali na usafiri wa ndege kwenda huko si wa uhakika.
.
Arsenal na Chelsea zimepewa tiketi 6000 kila moja kwa ajili ya mashabiki , wakati uwanja wa fainali ukiingiza karibia mashabiki 70,000.
.
UEFA wameeleza sababu za kutoa tiketi hizo chache kwa timu hizo, wamedai mji wa Baku hauwezi kumudu wingi wa mashabiki zaidi ya 15,000.
.
Katibu mkuu wa chama cha soka cha Azerbaijan akimjibu Klopp amesema : “ Nimeshangazwa sana na kauli zake.Mara zote amekuwa ni mtu mwenye mawazo chanya. Zaidi ya hayo,Wote tunajua ni mtu ambaye amepata matokeo mazuri sana katika soka,”
.
“Lakini katika hili, ninapinga vikali maoni yake kwamba soka liwe na mipaka ya Kijiografia”
.
Tunatakiwa kuheshimu na kukuza thamani ya mpira wa miguu. Na moja ya thamani kubwa ni kupanua mipaka ya mpira wa miguu na utandawazi wake” Amesema Elkhan Mammadov.
.
Mammadov ameongeza kuwa, kuchezwa kwa fainai hizo za Ulaya katika nchi za Ulaya mashariki zinafungua fursa za kukuza mchezo huo na kuvutia vijana wadogo wajihusishe nao.