Wazazi wa Curry walichoamua kuhusu watoto wao
Seth Curry anacheza Blazers, huku kaka yake ambaye ni Steph Curry anacheza Warriors.
Wakati wa mechi za Playoffs zinaendelea wazazi wao Dell na Sonya wamekuwa wakihudhuria kwenye mechi zao kuwashangilia watoto wao. Steph akiwa anacheza wanaenda uwanjani kumshangilia , baada ya hapo wanakwea pipa kwenda kumuangalia Seth akiwa timu yake ya Blazers.
Sasa Warriors na Blazers wote wamefuzu fainali ya Western Conference, hivyo Steph na Seth wanaenda kukutana.
Swali likaja, Je wazazi wao watamshangilia nani katika fainali hiyo?.
Dell na Sonya wameeleza ni nini watafanya. Wamesema kuwa watarusha shilingi na hivyo shilingi itaamua ni mzazi yupi atamshangilia mtoto yupi.