Herrera kutua kwa matajiri wa Ufaransa
Imeripotiwa kuwa kiungo Mhispania Ander Herrera atajiunga na klabu ya PSG ya Ufaransa baada ya jana kuthibitisha kuwa anaondoka Man United aliyoicheza kwa muda wa miaka mitano. Herrera, 29, anaondoka akiwa mchezaji huru kufuatia mkataba wake kumalizika majira ya kiangazi mwaka huu. Katika hiyo miaka mitano akiwa na United, Herrera amefunga magoli 20 kwenye mechi …