Beno Kalolanya amalizana na Yanga
Aliyekuwa kipa wa Klabu ya Yanga Beno kakolanya amemalizana na Klabu hiyo baada ya muda mrefu kupita tangu aombe kuondoka katika Klabu hiyo.
Beno amesema kuwa anamshukuru Mungu zoezi hilo limemalizika tayari ashamalizana na Yanga na sasa ni mchezaji huru.
.
“Mimi najisikia vizuri kumalizana na Yanga na nawashukuru kwa ushirikiano walionionyesha toka nimeingia Yanga. Sasa naenda kuanza maisha sehemu nyingine, na sasa ni mchezaji huru , bado sijaanza mazungumzo na klabu yoyote ile” amesema Kakolanya