Berbatov awakataa Tottenham, moyo wake upo Manchester
Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Bulgaria na vilabu vya Tottenham Hotspurs na Manchester United vya England Dimitar Berbatov (38) ameonesha kuwa pamoja na kuwa amewahi kuvichezea vilabu vyote vya Tottenham na Manchester United lakini yeye anaipenda zaidi Manchester United.
Berbatov ameeleza kuwa kama anapewa nafasi ya kurudi uwanjani kucheza na akapewa nafasi ya kuamua kurudi kati ya Tottenham na Man United basi ataamua kurudi Man United licha ya kuwa Tottenham anakubali kuwa wana uwanja mzuri na wamejihakikishia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao lakini yeye ataenda Man United.
.
‘Ni beji, historia, wachezaji wakubwa waliopita, Old Trafford, na nguvu ya mvuto waliyonayo.’ Alieleza Dimitar vitu vinavyomuita Man United huku akieleza kuwa licha ya kuwa wapo vibaya lakini anaamini watashinda mataji ndani ya miaka mitano.
.
“ Spurs inacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, wana uwanja wao mpya, wana uwanja mzuri wa mazoezi na wachezaji bora kwa sasa lakini mwisho wa siku ningeichagua kuichezea Manchester United” Berbatov alipohojiwa na dailymail na kueleza mawazo yake wapi anapenda kucheza
Berbatov ameicheza Tottenham kwa misimu miwili tu baada ya kujiunga nayo 2006 akitokea Bayer Leverkusen na 2008 akatimkia Man United na kuicha Tottenham akiwa kaichezea michezo 70 na kufunga mabao 27 wakati Man United aliyodumu kwa miaka minne (2008-2012) aliichezea michezo 108 na kupachika nyavuni mabao 48.