Samatta abeba tuzo barani Ulaya
Mshambuliaji wa klabu ya Genk Mtanzania Mbwana Samatta ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa kiafrika au mwenye asili ya Afrika anayecheza nchini Ubelgiji ‘Ebony Shoe Award’
.
Nahodha wa Man City Vincent Kompany ashawahi kushinda tuzo hiyo mara mbili.
Samatta hata hivyo hakuweza kuhudhuria sherehe za ugawaji wa tuzo hizo, kupitia mtandao wa Twitter alieleza ameshindwa kuhudhuria kutokana na sababu zisizotarajiwa na zilizo nje ya uwezo wake.
Samatta amekuwa ni mchezaji watatu wa Genk kuwahi kushinda tuzo hiyo.