Msimlishe Zizou maneno kuhusu Pogba
Ligi Kuu mbalimbali barani Ulaya zikielekea kumalizika huku tetesi za usajili zikiendelea kutamba kuhusiana na wachezaji mbalimbali kuhusishwa kuwa mbioni kuvihama vilabu vyao na kwenda kwingi, suala la kiungo wa Manchester United Paul Pogba kuhusishwa na Real Madrid ni kubwa zaidi.
.
Paul Pogba ambaye amewahi kutoa kauli inayoashiria kuwavutia Real Madrid kuongeza nguvu ya kumuhitaji, ameanza kuhusishwa na kwenda Real Madrid kwa zaidi ya miezi miwili hasa baada ya kutamka kuwa ni furaha na ndoto ya kijana yoyote kwenda kucheza Real Madrid chini ya kocha Zidane.
.
Baada ya taarifa hizo na Zidane kuonekana akimsifia, alipoulizwa kuhusiana na klabu yake anayoinoa ya Real Madrid kuwa mbioni Paul Pogba ameeleza kuwa ni mchezaji mzuri lakini ni suala la mapema kusema ni nani anafuatia au nani anaondoka.
.
“Nilisema Paul Pogba ni mchezaji mzuri lakini ningeweza kusema hivyo hivyo pia kwa wachezaji wengine, mwisho wa msimu ndio tutajua mchezaji gani anakuja hapa (Real Madrid) na nani anaondoka lakini sijasema kuwa tunaenda kumsajili Paul Pogba ” alisema Zidane alipohojiwa na ESPN