Arrizabalaga ajutia kumgomea kocha wake
Wakati mlinda mlango wa Chelsea Kepa Arrizabalaga ana msimu mmoja tu katika klabu ya Chelsea aliyojiunga nayo 2018 akitokea Athletic Bilbao ya nchini kwao Hispania, ukiachana na uwezo wake anaouonesha uwanjani alikuwa gumzo kubwa gumzo kubwa baada ya kumgomea kocha wake Maurizio Sarri hadharani.
Zikiwa zimepita wiki 10 toka Kepa Arrizabalaga agome kufanyiwa mabadiliko katika mchezo wa fainali Carabao Cup ili aingie Willy Caballero kuchukua nafasi yake, Kepa Arrizabalaga aligoma na kuwashangaza wengi kiasi cha baadae kuamua uomba radhi lakini klabu yake ya Chelsea ili muadhibu kwa kumpiga faini.
.
“Ndio ilikuwa habari iliyotawala duniani watu walikuwa wanaizungumzuia na wanaizungumzia kwa ubaya ni kawaida kwa watu kuongea.
Baada ya lile tukio baba yangu alizungumza na mimi tulipokuwa nyumbani lakini hakuhitaji kusema maneno mengi kwangu mimi”
.
“Tukio lilitokea Jumapili na Jumatano sikupangwa kucheza dhidi ya Tottenham hadi niliporudi kwenye mchezo wa Fullham, nilifanya kitu ambacho sijivunii
na ulikuwa ni wakati mgumu ambao nilitumia kujifunza, kwa sasa ni muda wa mimi kusonga mbele, niliomba msamaha maisha yanabidi yaendelee wote tunafanya makosa.”
Iliripotiwa kuwa pamoja na kuwa Kepa alikuwa anacheza vizuri lakini kocha Maurizio Sarri alitaka kumtoa Kepa dakika ya 119 katika mchezo huo wa fainali ya Carabao Cup dhidi ya Manchester City ili aingie Willy Caballero ambaye ana rekodi nzuri ya kucheza penati ila Kepa aligoma na kwenda kushindwa kucheza mikwaju ya penati na hatimae timu yake ikaishia kupoteza kwa penati 4-3.