Mshindi wa Ballon d’Or aachwa timu ya Taifa
Habari inayosisimua kwa sasa katika soka la wanawake ni kuhusiana na mchezaji bora wa dunia wa Ballon d’Or Ada Hegerberg kutojumuishwa katika kikosi cha timu yake ya taifa ya wanawake ya nchini Norway, kitendo ambacho kimewashangaza wengi na kuanza kujiuliza.
.
Inadaiwa kuachwa kwa mchezaji huyo katika timu ya taifa ya wanawake ya Norway kunatokana na Ada kuwa katika mvutano na shirikisho la soka la Norway kuhusiana na uendeshaji wa soka la wanawake na kukosekana kwa heshima kwa wachezaji wanawake nchini Norway, hivyo inadaiwa ameachwa kama kukomolewa sio kwa uwezo.
.
Ada ambaye hajaitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya wanawake kitakachocheza fainali za Kombe la Dunia June 2019, aligoma kuichezea timu yake ya taifa ya Norway toka 2017 kwa madai kuwa hakuna heshima nchini Norway kwa wachezaji wanawake.
Ada kwa sasa anaichezea klabu ya Lyon ya nchini Ufaransa akiwa na umri wa miaka 23.
.
“Tulijaribu kukaa nae na kutatua matatizo yaliyokuwepo lakini aliamua kutokucheza, kama kocha unatakiwa kuangalia wachezaji ambao wanataka kuwa sehemu ya timu Ada hataki, tuna heshimu hilo na tutacheza kwa juhudi tukiwa na wachezaji wengine” alisema Martin Sjogren kocha wa timu ya taifa ya Norway ya Wanawake