Azam fc yaahidi kutinga fainali kombe la FA
Kuelekea mchezo wa nusu fainali wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup, msemaji wa Azam FC Jaffar Iddi Maganga amesema kuwa katika mchezo huo watahakikisha wanafanya vizuri na kutinga fainali ya mashindano hayo.
Mchezo huo utachezwa kesho saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.
Maganga amesema kuwa mchezo huo kwao wanauchukulia ni fainali na wanaiheshimu KMC kwa hatua iliyofikia katika mashindano hayo.
.
“Kwetu sisi kama Azam FC tunaona mchezo wa kesho kama mchezo wa fainali kwetu,tunaiheshimu KMC kwa hatua iliyofikia katika mashindano hayo, tuna matumaini kwa benchi letu la Ufundi na wachezaji wetu wanatambua nini cha kufanya kesho ili tuweze kupata nafasi ya kusonga mbele katika mashindano hayo” Maganga
Viingilio katika mchezo huo ni elfu 3000 na Elfu 5000.