Azam fc yaahidi kutinga fainali kombe la FA
Kuelekea mchezo wa nusu fainali wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup, msemaji wa Azam FC Jaffar Iddi Maganga amesema kuwa katika mchezo huo watahakikisha wanafanya vizuri na kutinga fainali ya mashindano hayo. Mchezo huo utachezwa kesho saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam. …