Bailly kuikosa AFCON Misri mwaka huu
Nyota tegemeo wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Manchester United Eric Bailly aliyeumia katika mchezo dhidi ya Chelsea Jumapili iliyopita atakuwa nje ya uwanja kwa muda wote wa msimu uliobaki kufuatia kuumia goti lake la kulia.
Bailly anashindwa kumaliza msimu kutokana na kuumia goti lake la kulia kwa kugongana na Marco Alonso dakika ya 71 na kushindwa kumalizia mchezo huo uliohitimika kwa sare ya kufungana 1-1.
Imeelezwa kuwa beki huyo ataikosa michuano ya AFCON itakayoanza Juni 21 mwaka huu nchini Misri, timu yake italazimika kutafuta mbadala wake anayeweza kupambana na kasi za washambuliaji wa timu za Namibia, Afrika ya Kusini pamoja na Morocco ambao wamepangwa Kundi D pamoja na Ivory Coast.