Suarez amvulia kofia Sterling
Nyota wa FC Barcelona ya nchini Hispania Luis Suarez na nyota wa klabu ya Manchester City ya nchini England Raheem Sterling wamewahi kucheza pamoja kwa miaka miwili wote wakiitumikia klabu ya Liverpool ya England, Suarez sasa ameonesha wazi wazi kufurahi kuimarika kwa Raheem Sterling.
Suarez amekiri kuwa Sterling mwenye umri wa miaka 24 amekuwa akiimarika kila kukicha na sio kama alivyokuwa Liverpool wakati ule wanacheza pamoja na kumtania kutokana alikuwa anaweza kukosa hata goli akiwa karibu na golikipa kwa sababu alikuwa hajui kumalizia.
.
“Raheem Sterling amekuwa akiimarika na kuendelea kukua kwa kipaji chake, nakumbuka tulikuwa tukimtania kuwa hajui kumalizia (kufunga) anaweza akawa yeye na golikipa lakini akakosa mpira ,atapaisha, tulikuwa tunamcheka sana” Luis Suarez kupitia Daily Mail akiongea kuhusiana na uwezo wa Raheem Sterling