Sarri ashangazwa Hazard kutokuwepo katika kikosi bora cha msimu England
Hivi karibuni kimetangazwa kikosi bora cha msimu huu ligi kuu England cha chama cha wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini England PFA, kikosi hicho kwa asilimia kubwa kimetawaliwa na majina ya wachezaji kutoka Manchester City na Liverpool ambao wanachuana vikali kutwaa taji hilo.
Jina la mchezaji ambaye yupo nje ya timu zinazowania Ubingwa wa EPL ni Paul Pogba wa Manchester United pekee lakini Manchester City wakitawala kwa kutoa wachezaji 6 katika orodha hiyo na Liverpool wachezaji wanne.
Baada ya kutotajwa kwa jina la nyota wa Chelsea Eden Hazard ambapo kocha wake Maurizio Sarri anaamini alistahili kuwemo katika orodha hiyo amesema kikosi hicho kimepangwa kwa kuzingatia msimamo wa EPL na sio ubora wa mchezaji mmoja mmoja.
.
“Nafiriki Eden Hazard anastahili kuwa katika kikosi bora cha Ligi Kuu England chenye wachezaji 11 lakini nafikiri pia kwa sasa msimamo upo wazi, kuna Manchester City na kuna Liverpool na kuna timu nyingine sasa naamini kura zimepigwa kwa ushawishi wa msimamo wa (EPL) ulivyo” alisema Sarri alipohojiwa na Espn
Wachezaji waliopo wa Liverpool ni Virgil van Dijk, Sadio Mane, Robertson na Alexander Arnold wakati Man City wakiwa sita Sergio Aguero, Raheem Sterling, Benardo Silva, Fernandinho, Laporte na kipa Ederson.