Kwa nini fainali ya Klabu Bingwa Afrika huchezwa mara mbili?
Moja kati ya vitu ambavyo mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu wamekuwa wakivilalamikia katika mashindano ya klabu Bingwa Afrika na Kombe la shirikisho Afrika, uamuzi wa michezo ya fainali kuchezwa mara mbili kama michezo ya hatua ya makundi au robo fainali na nusu fainali.
Kupitia Azam TV wameongea na Rais wa shirikisho la mpira wa mguu Afrika CAF Ahmad Ahmad na kumuuliza kuhusiana na utaratibu huo, hawaoni kama inapoteza mvuto? Kwa nini wasiige mfano wa michuano kama ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo imekuwa ikichezwa fainali katika mji mmoja ambao huchaguliwa mapema?
.
“Unajua Ulaya wameelimika sana kuhusu mpira hawaoni kuwa hii timu imetoka sehemu nyingine au imetoka sehemu gani wanaona mpira ni mpira unaowavutia lakini Afrika wanaangalia timu kwa mfano hapa Tanzania, ukileta timu kutoka nje hawatovutika uwanjani ,wanapenda Simba kama ukiweka mechi ya Simba uwanja utajaa, hilo linatufanya tushindwe kufanya maamuzi kuweka fainali ya mechi moja. Unajua sio jambo la kawaida kufuata mifano ya Ulaya” Rais wa CAF Ahmad Ahmad akiongea na Azam TV