KMC watuma salamu kwa Simba, wasema kiporo kimeshachacha
Kuelekea mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara ambao ni kiporo utakaowakutanisha KMC na Simba SC kesho April 25 saa 10.00 jioni katika Uwanja wa CCM,msemaji wake Anwar Binde amesema kuwa kiporo hicho tayari kimeshachacha na hakiliki kwa Simba.
Msemaji huyo amesema kuwa kikosi hicho cha wachezaji 20 tayari kipo jijini Mwanza kwa ajili ya kukabiliana na Wekundu hao wa Msimbazi.
KMC wanatumia uwanja wa CCM Kirumba kama uwanja wao wa nyumbni.
Binde ameongeza kuwa japo Simba ni timu kubwa wanaiheshimu na hawaiogopi hivyo ushindi katika mechi ya kesho ni muhimu na wanaamini watafanya vizuri katika mchezo huo.
.
” Tunamshukuru Mungu wachezaji wetu wako na hali nzuri na morali ya kutosha kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya Simba SC, tunafahamu uwezo wa Simba lakini katika mchezo wa kesho tutafanya vizuri na mpaka sasa kiporo kishachacha na hakiliki tena” amesema Binde