Waziri Kigwangalla amualika shabiki wa Man City Tanzania
Jina la mtoto Braydon Bent raia wa Uingereza ambaye ni shabiki mkubwa wa timu ya Manchester City linaonekana kuzidi kupata umaarufu mkubwa duniani kote sio tu kutokana na ushabiki wake wa Manchester City ila ni uelewa wake wa soka kuwa mkubwa ukilinganisha na umri wake.
Braydon kwa sasa ana umri wa miaka 10 na amekuwa mara kadhaa kutokana na kufahamu kuwa ana mashabiki Tanzania, wakati mwingine amekuwa akipost video akiongea lugha ya kiswahili hasa akiwa anaongelea mechi za huko barani Ulaya.
Amekuwa akiwatakia kheri ya sikukuu mbalimbali kama mwaka mpya watanzania na watu wa Afrika Mashariki kwa lugha ya Kiswahili.
Baada ya waziri wa maliasili na Utalii Dr.Hamis Kigwangalla kuona video ya Braydon akiwatakia watanzania sikukuu njema ya Pasaka kwa lugha ya kiswahili huku akivitaja vivutio vya utalii Tanzania, Waziri Kigwangalla akaamua kupost video hiyo katika akaunti yake ya instagram na kumshukuru huku akitaka kumpa ubalozi.
.
“Ahsante Braydon Bent ,kama waziri wa maliasili na utalii wa Tanzania, ningependa kukualika Tanzania kwa gharama zetu na kukuteua kuwa balozi wetu wa hiari….. ” aliandika Waziri Kigwangalla