Rashford avujisha mbinu za Solskjaer kwa Barca
Picha za video zimemnasa mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford akifanya uzembe wakati wa mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Barcelona iliyomalizika kwa Barcelona kuondoka na ushindi wa mabao 3-0 katika dimba lao la Camp Nou.
Rashford kuna wakati mchezo huo ukiendelea aliitwa na kocha wake Ole Gunnar Solskjaer na kumpa kikaratasi cha maelekezo ili awaambie wenzake wabadilishe mfumo lakini alipoingia nacho uwanjani inadaiwa kabla hata ya kuwaelekeza wenzake alikiangusha kikaratasi kwa mlinda mlango wa Barcelona akakiokota.
Mlinda mlango wa Barcelona Ter Stegen baada ya kukiokota na kukisoma alitambua wazi mbinu za wapinzani wao, hivyo inadaiwa kuna uwezekano mkubwa Rashford alifelisha mfumo huo kwa kuangusha mbinu zao jirani na mpinzani wao ndio maana mfumo haukuwa na madhara.