Wanyama aifukuzia rekodi ya kaka yake Klabu Bingwa Ulaya
Kiungo wa timu ya Tottenham Hotspur ambaye pia ni raia wa Kenya Victor Wanyama yuko mbioni kuinyemelea rekodi ya kaka yake wa damu ambaye pia alikuwa mchezaji wa zamani wa Inter Milan ya nchini Italia Mc Donald Mariga aliyekuwa akifundishwa na Mourinho wakati huo.
McDonald Mariga ndio mchezaji pekee wa Afrika Mashariki aliyewahi kufika hatua ya fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Inter Milan na kutwa taji hilo, kabla ya hapo hakukuwa na mchezaji yoyote Afrika Mashariki ambaye aliwahi kufikia hatua hiyo.
Tukio hilo la kihistoria lilitokea 2010 na kuweka rekodi, baada ya Mariga sasa kuna uwezekano ndugu yake akawa mchezaji wa pili wa Afrika Mashariki baada ya kaka yake Mariga kuwahi kufikia hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kama Victor Wanyama na timu yake ya Tottenham wataiotoa Ajax katika mchezo wa nusu fainali.
Wanyama jana alikuwa sehemu ya timu ya Tottenham Hotspur iliyofanikiwa kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwatoa Manchester, licha ya kupoteza kwa goli 4-3 ila Tottenham walifuzu kwa faida ya magoli ya ugenini baada ya timu hizo kufungana jumla ya goli 4-4 kwa mechi zote mbili.