Yondani na Fei Toto kuwakosa Mtibwa kesho
Mlinzi wa Yanga Kelvin Yondani na Kiungo Feisal Salum hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa saa 8.00 mchana kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Yondani alipata kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar, Feisal Salum ana kadi tatu za njano ,hivyo wote wanatumikia adhabu hizo.
Mratibu wa Klabu hiyo Hafidhi Salehe amesema kuwa kuwakosa wachezaji hao kutakuwa na pengo lakini Ibrahim Ajibu na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ washarejea kikosini na kesho watakuwa sehemu ya kikosi kitakacho cheza kesho.
.
” Kuwakosa Yondani na Feisal naweza kusema kutakuwa na pengo lakini nafasi zao zitazibwa maana Ninja baada ya kumaliza adhabu yake tayari yupo kikosini na Ajib pia baada ya kupona majeraha yake nae tunae kikosini, hivyo naamini tutafanya vizuri katika mchezo wetu wa kesho” Salehe
Salehe ameongeza kuwa mchezo wao wa kesho utachezwa saa nane mchana ili kutoa nafasi kwa watanzania waweze kuitazama michuano ya Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 inayoendelea kuchezwa jijini Dar es Salaam ambapo Tanzania ndio mwenyeji wa michuano hiyo.
.
” Tumepata taarifa kuwa mechi zote za Ligi kuu zitakazochezwa kesho zitacheza saa 8.00 mchana kwa sababu ya kutoa nafasi kuitazama michuano ya AFCON U17 inayoendelea kuchezwa jijini Dar es Salaam “amesema Salehe